Back to Languages

Swahili - Chapter 6 - Al-Anam

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 130 — Surah Al-Anam 6:130

Enyi makundi ya majini na watu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii. Nao watasema: Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri