Back to Languages

    Swahili - Chapter 75

    Translation by Ali Muhsin Al Barwani

    Verse 1

    Ninaapa kwa Siku ya Kiyama

    Verse 2

    Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu

    Verse 3

    Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake

    Verse 4

    Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake

    Verse 5

    Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake

    Verse 6

    Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama

    Verse 7

    Basi jicho litapo dawaa

    Verse 8

    Na mwezi utapo patwa

    Verse 9

    Na likakusanywa jua na mwezi

    Verse 10

    Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio

    Verse 11

    La! Hapana pa kukimbilia

    Verse 12

    Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu

    Verse 13

    Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha

    Verse 14

    Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake

    Verse 15

    Na ingawa atatoa chungu ya udhuru

    Verse 16

    Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka

    Verse 17

    Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha

    Verse 18

    Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake

    Verse 19

    Kisha ni juu yetu kuubainisha

    Verse 20

    Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani

    Verse 21

    Na mnaacha maisha ya Akhera

    Verse 22

    Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara

    Verse 23

    Zinamwangallia Mola wao Mlezi

    Verse 24

    Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana

    Verse 25

    Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo

    Verse 26

    La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo

    Verse 27

    Na pakasemwa: Nani wa kumganga

    Verse 28

    Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki

    Verse 29

    Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi

    Verse 30

    Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi

    Verse 31

    Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali

    Verse 32

    Bali alikanusha, na akageuka

    Verse 33

    Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao

    Verse 34

    Ole wako, ole wako

    Verse 35

    Kisha Ole wako, ole wako

    Verse 36

    Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure

    Verse 37

    Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa

    Verse 38

    Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo

    Verse 39

    Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke

    Verse 40

    Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu