Back to Languages
Swahili - Chapter 77
Translation by Ali Muhsin Al Barwani
Verse 1
Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole
Verse 2
Na zinazo vuma kwa kasi
Verse 3
Na zikaeneza maeneo yote
Verse 4
Na zinazo farikisha zikatawanya
Verse 5
Na zinazo peleka mawaidha
Verse 6
Kwa kuudhuru au kuonya
Verse 7
Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa
Verse 8
Wakati nyota zitakapo futwa
Verse 9
Na mbingu zitakapo pasuliwa
Verse 10
Na milima itakapo peperushwa
Verse 11
Na Mitume watakapo wekewa wakati wao
Verse 12
Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo
Verse 13
Kwa siku ya kupambanua
Verse 14
Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini
Verse 15
Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha
Verse 16
Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia
Verse 17
Kisha tukawafuatilizia walio fuatia
Verse 18
Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu
Verse 19
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha
Verse 20
Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa
Verse 21
Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti
Verse 22
Mpaka muda maalumu
Verse 23
Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria
Verse 24
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha
Verse 25
Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
Verse 26
Walio hai na maiti
Verse 27
Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu
Verse 28
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha
Verse 29
Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha
Verse 30
Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu
Verse 31
Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako
Verse 32
Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba
Verse 33
Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano
Verse 34
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha
Verse 35
Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu
Verse 36
Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru
Verse 37
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha
Verse 38
Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia
Verse 39
Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi
Verse 40
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha
Verse 41
Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem
Verse 42
Na matunda wanayo yapenda
Verse 43
Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda
Verse 44
Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema
Verse 45
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha
Verse 46
Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu
Verse 47
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha
Verse 48
Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami
Verse 49
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha
Verse 50
Basi maneno gani baada ya haya watayaamini