Back to Languages

Swahili - Chapter 80 - Abasa

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah Abasa 80:1

Alikunja kipaji na akageuka

Verse 2 — Surah Abasa 80:2

Kwa sababu alimjia kipofu

Verse 3 — Surah Abasa 80:3

Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika

Verse 4 — Surah Abasa 80:4

Au atawaidhika, na mawaidha yamfae

Verse 5 — Surah Abasa 80:5

Ama ajionaye hana haja

Verse 6 — Surah Abasa 80:6

Wewe ndio unamshughulikia

Verse 7 — Surah Abasa 80:7

Na si juu yako kama hakutakasika

Verse 8 — Surah Abasa 80:8

Ama anaye kujia kwa juhudi

Verse 9 — Surah Abasa 80:9

Verse 10 — Surah Abasa 80:10

Verse 11 — Surah Abasa 80:11

Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana

Verse 12 — Surah Abasa 80:12

Basi anaye penda akumbuke

Verse 13 — Surah Abasa 80:13

Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa

Verse 14 — Surah Abasa 80:14

Zilizo inuliwa, zilizo takaswa

Verse 15 — Surah Abasa 80:15

Zimo mikononi mwa Malaika waandishi

Verse 16 — Surah Abasa 80:16

Verse 17 — Surah Abasa 80:17

Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha

Verse 18 — Surah Abasa 80:18

Kwa kitu gani amemuumba

Verse 19 — Surah Abasa 80:19

Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria

Verse 20 — Surah Abasa 80:20

Kisha akamsahilishia njia

Verse 21 — Surah Abasa 80:21

Kisha akamfisha, akamtia kaburini

Verse 22 — Surah Abasa 80:22

Kisha apendapo atamfufua

Verse 23 — Surah Abasa 80:23

La! Hajamaliza aliyo muamuru

Verse 24 — Surah Abasa 80:24

Hebu mtu na atazame chakula chake

Verse 25 — Surah Abasa 80:25

Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu

Verse 26 — Surah Abasa 80:26

Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu

Verse 27 — Surah Abasa 80:27

Kisha tukaotesha humo nafaka

Verse 28 — Surah Abasa 80:28

Na zabibu, na mimea ya majani

Verse 29 — Surah Abasa 80:29

Na mizaituni, na mitende

Verse 30 — Surah Abasa 80:30

Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara

Verse 31 — Surah Abasa 80:31

Na matunda, na malisho ya wanyama

Verse 32 — Surah Abasa 80:32

Kwa manufaa yenu na mifugo yenu

Verse 33 — Surah Abasa 80:33

Basi utakapo kuja ukelele

Verse 34 — Surah Abasa 80:34

Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye

Verse 35 — Surah Abasa 80:35

Verse 36 — Surah Abasa 80:36

Verse 37 — Surah Abasa 80:37

Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha

Verse 38 — Surah Abasa 80:38

Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri

Verse 39 — Surah Abasa 80:39

Zitacheka, zitachangamka

Verse 40 — Surah Abasa 80:40

Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi

Verse 41 — Surah Abasa 80:41

Giza totoro litazifunika

Verse 42 — Surah Abasa 80:42

Hao ndio makafiri watenda maovu