Back to Languages

    Swahili - Chapter 81

    Translation by Ali Muhsin Al Barwani

    Verse 1

    Jua litakapo kunjwa

    Verse 2

    Na nyota zikazimwa

    Verse 3

    Na milima ikaondolewa

    Verse 4

    Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe

    Verse 5

    Na wanyama wa mwituni wakakusanywa

    Verse 6

    Na bahari zikawaka moto

    Verse 7

    Na nafsi zikaunganishwa

    Verse 8

    Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa

    Verse 9

    Kwa kosa gani aliuliwa

    Verse 10

    Na madaftari yatakapo enezwa

    Verse 11

    Na mbingu itapo tanduliwa

    Verse 12

    Na Jahannamu itapo chochewa

    Verse 13

    Na Pepo ikasogezwa

    Verse 14

    Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha

    Verse 15

    Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma

    Verse 16

    Zinazo kwenda, kisha zikajificha

    Verse 17

    Na kwa usiku unapo pungua

    Verse 18

    Na kwa asubuhi inapo pambazuka

    Verse 19

    Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu

    Verse 20

    Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi

    Verse 21

    Anaye t'iiwa, tena muaminifu

    Verse 22

    Na wala huyu mwenzenu hana wazimu

    Verse 23

    Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi

    Verse 24

    Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu

    Verse 25

    Wala hii si kauli ya Shetani maluuni

    Verse 26

    Basi mnakwenda wapi

    Verse 27

    Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote

    Verse 28

    Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa

    Verse 29

    Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote

    Unexpected Application Error!

    Unexpected token '<', "<!DOCTYPE "... is not valid JSON

    SyntaxError: Unexpected token '<', "<!DOCTYPE "... is not valid JSON