Back to Languages
Swahili - Chapter 97
Translation by Ali Muhsin Al Barwani
Verse 1
Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu
Verse 2
Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri
Verse 3
Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu
Verse 4
Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo
Verse 5
Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri