Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 112 - Al-Ikhlas
Translation by Abdullah Muhammad Abu Bakr — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Ikhlas 112:1
Sema, ewe Mtume, «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na Sifa, Asiye na mshirika katika hayo
Verse 2 — Surah Al-Ikhlas 112:2
«Mwenyezi Mungu Ambaye Peke Yake Ndiye Mwenye kukusudiwa kwa kukidhi haja na matakwa
Verse 3 — Surah Al-Ikhlas 112:3
«Hana mwana wala mzazi wala mke
Verse 4 — Surah Al-Ikhlas 112:4
«Wala hakuna yoyote katika viumbe Vyake mwenye kufanana wala kushabihiyana na Yeye katika Majina Yake, Sifa Zake wala vitendo Vyake.»