Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 100 - Al-Adiyat
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Adiyat 100:1
Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua
Verse 2 — Surah Al-Adiyat 100:2
Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini
Verse 3 — Surah Al-Adiyat 100:3
Wakishambulia wakati wa asubuhi
Verse 4 — Surah Al-Adiyat 100:4
Huku wakitimua vumbi
Verse 5 — Surah Al-Adiyat 100:5
Na wakijitoma kati ya kundi
Verse 6 — Surah Al-Adiyat 100:6
Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi
Verse 7 — Surah Al-Adiyat 100:7
Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo
Verse 8 — Surah Al-Adiyat 100:8
Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali
Verse 9 — Surah Al-Adiyat 100:9
Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini
Verse 10 — Surah Al-Adiyat 100:10
Na yakakusanywa yaliomo vifuani
Verse 11 — Surah Al-Adiyat 100:11
Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote