Back to Languages

Swahili - Chapter 2 - Al-Baqarah

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 126 — Surah Al-Baqarah 2:126

Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Akasema: Na mwenye kukufuru pia nitamstarehesha kidogo, kisha nitamsukumiza kwenye adhabu ya Moto, napo ni pahala pabaya mno pa kurejea