Back to Languages

Swahili - Chapter 20 - Ta-Ha

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 47 — Surah Ta-Ha 20:47

Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani itakuwa juu ya aliye fuata uwongofu