Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter
Swahili - Chapter 50 - Qaf
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Qaf 50:1
Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu
Verse 2 — Surah Qaf 50:2
Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: Hili ni jambo la ajabu
Verse 3 — Surah Qaf 50:3
Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali
Verse 4 — Surah Qaf 50:4
Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinacho hifadhi yote
Verse 5 — Surah Qaf 50:5
Lakini waliikanusha Haki ilipo wajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mkorogo
Verse 6 — Surah Qaf 50:6
Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa
Verse 7 — Surah Qaf 50:7
Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna
Verse 8 — Surah Qaf 50:8
Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea
Verse 9 — Surah Qaf 50:9
Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa
Verse 10 — Surah Qaf 50:10
Na mitende mirefu yenye makole yaliyo zaa kwa wingi
Verse 11 — Surah Qaf 50:11
Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyo kuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyo kuwa ufufuaji
Verse 12 — Surah Qaf 50:12
Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakaazi wa Rassi na Thamudi
Verse 13 — Surah Qaf 50:13
Na A'di na Firauni na kaumu ya Lut'i
Verse 14 — Surah Qaf 50:14
Na wakaazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao
Verse 15 — Surah Qaf 50:15
Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza. Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya
Verse 16 — Surah Qaf 50:16
Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake
Verse 17 — Surah Qaf 50:17
Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni
Verse 18 — Surah Qaf 50:18
Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari
Verse 19 — Surah Qaf 50:19
Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyo kuwa ukiyakimbia
Verse 20 — Surah Qaf 50:20
Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi
Verse 21 — Surah Qaf 50:21
Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi
Verse 22 — Surah Qaf 50:22
(Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo tumekuondolea pazia lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali
Verse 23 — Surah Qaf 50:23
Na mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha tayarishwa
Verse 24 — Surah Qaf 50:24
Mtupeni katika Jahannamu kila kafiri mwenye inda
Verse 25 — Surah Qaf 50:25
Akatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka
Verse 26 — Surah Qaf 50:26
Aliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali
Verse 27 — Surah Qaf 50:27
Mwenzake aseme: Ee Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali
Verse 28 — Surah Qaf 50:28
(Mwenyezi Mungu) aseme: Msigombane mbele yangu. Nilikuleteeni mbele onyo langu
Verse 29 — Surah Qaf 50:29
Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu
Verse 30 — Surah Qaf 50:30
Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada
Verse 31 — Surah Qaf 50:31
Na Pepo italetwa karibu kwa ajili ya wachamngu, haitakuwa mbali
Verse 32 — Surah Qaf 50:32
Haya ndiyo mnayo ahidiwa kwa kila mwenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu na akajilinda
Verse 33 — Surah Qaf 50:33
Mwenye kumwogopa Mwingi wa Rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo ulio elekea
Verse 34 — Surah Qaf 50:34
(Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya daima dawamu
Verse 35 — Surah Qaf 50:35
Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada
Verse 36 — Surah Qaf 50:36
Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao walio kuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je! Walipata pa kukimbilia
Verse 37 — Surah Qaf 50:37
Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia
Verse 38 — Surah Qaf 50:38
Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu
Verse 39 — Surah Qaf 50:39
Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa
Verse 40 — Surah Qaf 50:40
Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu
Verse 41 — Surah Qaf 50:41
Na sikiliza siku atapo nadi mwenye kunadi kutoka pahala karibu
Verse 42 — Surah Qaf 50:42
Siku watakapo sikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka
Verse 43 — Surah Qaf 50:43
Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio marejeo
Verse 44 — Surah Qaf 50:44
Siku itapo wapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi
Verse 45 — Surah Qaf 50:45
Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur'ani anaye liogopa onyo