Back to Languages

Swahili - Chapter 7 - Al-Araf

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 74 — Surah Al-Araf 7:74

Na kumbukeni alivyo kufanyeni wa kushika pahala pa A'adi na akakuwekeni vizuri katika nchi, mnajenga majumba ya fakhari katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika milima. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu wala msitende uovu katika nchi kwa ufisadi