Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 90 - Al-Balad
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Balad 90:1
Naapa kwa Mji huu
Verse 2 — Surah Al-Balad 90:2
Nawe unaukaa Mji huu
Verse 3 — Surah Al-Balad 90:3
Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa
Verse 4 — Surah Al-Balad 90:4
Hakika tumemuumba mtu katika taabu
Verse 5 — Surah Al-Balad 90:5
Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza
Verse 6 — Surah Al-Balad 90:6
Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali
Verse 7 — Surah Al-Balad 90:7
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona
Verse 8 — Surah Al-Balad 90:8
Kwani hatukumpa macho mawili
Verse 9 — Surah Al-Balad 90:9
Na ulimi, na midomo miwili
Verse 10 — Surah Al-Balad 90:10
Na tukambainishia zote njia mbili
Verse 11 — Surah Al-Balad 90:11
Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani
Verse 12 — Surah Al-Balad 90:12
Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani
Verse 13 — Surah Al-Balad 90:13
Kumkomboa mtumwa
Verse 14 — Surah Al-Balad 90:14
Au kumlisha siku ya njaa
Verse 15 — Surah Al-Balad 90:15
Yatima aliye jamaa
Verse 16 — Surah Al-Balad 90:16
Au masikini aliye vumbini
Verse 17 — Surah Al-Balad 90:17
Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana
Verse 18 — Surah Al-Balad 90:18
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani
Verse 19 — Surah Al-Balad 90:19
Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni
Verse 20 — Surah Al-Balad 90:20
Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande