Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 91 - Ash-Shams
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Ash-Shams 91:1
Naapa kwa jua na mwangaza wake
Verse 2 — Surah Ash-Shams 91:2
Na kwa mwezi unapo lifuatia
Verse 3 — Surah Ash-Shams 91:3
Na kwa mchana unapo lidhihirisha
Verse 4 — Surah Ash-Shams 91:4
Na kwa usiku unapo lifunika
Verse 5 — Surah Ash-Shams 91:5
Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga
Verse 6 — Surah Ash-Shams 91:6
Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza
Verse 7 — Surah Ash-Shams 91:7
Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza
Verse 8 — Surah Ash-Shams 91:8
Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake
Verse 9 — Surah Ash-Shams 91:9
Hakika amefanikiwa aliye itakasa
Verse 10 — Surah Ash-Shams 91:10
Na hakika amekhasiri aliye iviza
Verse 11 — Surah Ash-Shams 91:11
Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao
Verse 12 — Surah Ash-Shams 91:12
Alipo simama mwovu wao mkubwa
Verse 13 — Surah Ash-Shams 91:13
Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake
Verse 14 — Surah Ash-Shams 91:14
Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa
Verse 15 — Surah Ash-Shams 91:15
Wala Yeye haogopi matokeo yake