Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 92 - Al-Layl
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Layl 92:1
Naapa kwa usiku unapo funika
Verse 2 — Surah Al-Layl 92:2
Na mchana unapo dhihiri
Verse 3 — Surah Al-Layl 92:3
Na kwa Aliye umba dume na jike
Verse 4 — Surah Al-Layl 92:4
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali
Verse 5 — Surah Al-Layl 92:5
Ama mwenye kutoa na akamchamngu
Verse 6 — Surah Al-Layl 92:6
Na akaliwafiki lilio jema
Verse 7 — Surah Al-Layl 92:7
Tutamsahilishia yawe mepesi
Verse 8 — Surah Al-Layl 92:8
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake
Verse 9 — Surah Al-Layl 92:9
Na akakanusha lilio jema
Verse 10 — Surah Al-Layl 92:10
Tutamsahilishia yawe mazito
Verse 11 — Surah Al-Layl 92:11
Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia
Verse 12 — Surah Al-Layl 92:12
Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu
Verse 13 — Surah Al-Layl 92:13
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia
Verse 14 — Surah Al-Layl 92:14
Basi nakuonyeni na Moto unao waka
Verse 15 — Surah Al-Layl 92:15
Hatauingia ila mwovu kabisa
Verse 16 — Surah Al-Layl 92:16
Anaye kadhibisha na kupa mgongo
Verse 17 — Surah Al-Layl 92:17
Na mchamngu ataepushwa nao
Verse 18 — Surah Al-Layl 92:18
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa
Verse 19 — Surah Al-Layl 92:19
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa
Verse 20 — Surah Al-Layl 92:20
Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa
Verse 21 — Surah Al-Layl 92:21
Naye atakuja ridhika