Back to Languages

Swahili - Chapter 82 - Al-Infitar

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Infitar 82:1

Mbingu itapo chanika

Verse 2 — Surah Al-Infitar 82:2

Na nyota zitapo tawanyika

Verse 3 — Surah Al-Infitar 82:3

Na bahari zitakapo pasuliwa

Verse 4 — Surah Al-Infitar 82:4

Na makaburi yatapo fukuliwa

Verse 5 — Surah Al-Infitar 82:5

Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma

Verse 6 — Surah Al-Infitar 82:6

Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu

Verse 7 — Surah Al-Infitar 82:7

Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha

Verse 8 — Surah Al-Infitar 82:8

Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga

Verse 9 — Surah Al-Infitar 82:9

Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo

Verse 10 — Surah Al-Infitar 82:10

Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu

Verse 11 — Surah Al-Infitar 82:11

Waandishi wenye hishima

Verse 12 — Surah Al-Infitar 82:12

Wanayajua mnayo yatenda

Verse 13 — Surah Al-Infitar 82:13

Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema

Verse 14 — Surah Al-Infitar 82:14

Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni

Verse 15 — Surah Al-Infitar 82:15

Wataingia humo Siku ya Malipo

Verse 16 — Surah Al-Infitar 82:16

Na hawatoacha kuwamo humo

Verse 17 — Surah Al-Infitar 82:17

Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani

Verse 18 — Surah Al-Infitar 82:18

Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani

Verse 19 — Surah Al-Infitar 82:19

Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu