Back to Languages

Swahili - Chapter 83 - Al-Mutaffifin

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Mutaffifin 83:1

Ole wao hao wapunjao

Verse 2 — Surah Al-Mutaffifin 83:2

Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe

Verse 3 — Surah Al-Mutaffifin 83:3

Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza

Verse 4 — Surah Al-Mutaffifin 83:4

Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa

Verse 5 — Surah Al-Mutaffifin 83:5

Katika Siku iliyo kuu

Verse 6 — Surah Al-Mutaffifin 83:6

Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 7 — Surah Al-Mutaffifin 83:7

Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin

Verse 8 — Surah Al-Mutaffifin 83:8

Verse 9 — Surah Al-Mutaffifin 83:9

Kitabu kilicho andikwa

Verse 10 — Surah Al-Mutaffifin 83:10

Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha

Verse 11 — Surah Al-Mutaffifin 83:11

Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo

Verse 12 — Surah Al-Mutaffifin 83:12

Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi

Verse 13 — Surah Al-Mutaffifin 83:13

Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale

Verse 14 — Surah Al-Mutaffifin 83:14

Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma

Verse 15 — Surah Al-Mutaffifin 83:15

Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi

Verse 16 — Surah Al-Mutaffifin 83:16

Kisha wataingia Motoni

Verse 17 — Surah Al-Mutaffifin 83:17

Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha

Verse 18 — Surah Al-Mutaffifin 83:18

Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin

Verse 19 — Surah Al-Mutaffifin 83:19

Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin

Verse 20 — Surah Al-Mutaffifin 83:20

Kitabu kilicho andikwa

Verse 21 — Surah Al-Mutaffifin 83:21

Wanakishuhudia walio karibishwa

Verse 22 — Surah Al-Mutaffifin 83:22

Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema

Verse 23 — Surah Al-Mutaffifin 83:23

Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia

Verse 24 — Surah Al-Mutaffifin 83:24

Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema

Verse 25 — Surah Al-Mutaffifin 83:25

Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri

Verse 26 — Surah Al-Mutaffifin 83:26

Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana

Verse 27 — Surah Al-Mutaffifin 83:27

Na mchanganyiko wake ni Tasniim

Verse 28 — Surah Al-Mutaffifin 83:28

Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa

Verse 29 — Surah Al-Mutaffifin 83:29

Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini

Verse 30 — Surah Al-Mutaffifin 83:30

Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana

Verse 31 — Surah Al-Mutaffifin 83:31

Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi

Verse 32 — Surah Al-Mutaffifin 83:32

Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea

Verse 33 — Surah Al-Mutaffifin 83:33

Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao

Verse 34 — Surah Al-Mutaffifin 83:34

Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri

Verse 35 — Surah Al-Mutaffifin 83:35

Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia

Verse 36 — Surah Al-Mutaffifin 83:36

Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda