Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 84 - Al-Inshiqaq
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Inshiqaq 84:1
Itapo chanika mbingu
Verse 2 — Surah Al-Inshiqaq 84:2
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza
Verse 3 — Surah Al-Inshiqaq 84:3
Na ardhi itakapo tanuliwa
Verse 4 — Surah Al-Inshiqaq 84:4
Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu
Verse 5 — Surah Al-Inshiqaq 84:5
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza
Verse 6 — Surah Al-Inshiqaq 84:6
Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta
Verse 7 — Surah Al-Inshiqaq 84:7
Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia
Verse 8 — Surah Al-Inshiqaq 84:8
Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi
Verse 9 — Surah Al-Inshiqaq 84:9
Na arudi kwa ahali zake na furaha
Verse 10 — Surah Al-Inshiqaq 84:10
Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake
Verse 11 — Surah Al-Inshiqaq 84:11
Basi huyo ataomba kuteketea
Verse 12 — Surah Al-Inshiqaq 84:12
Na ataingia Motoni
Verse 13 — Surah Al-Inshiqaq 84:13
Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake
Verse 14 — Surah Al-Inshiqaq 84:14
Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena
Verse 15 — Surah Al-Inshiqaq 84:15
Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona
Verse 16 — Surah Al-Inshiqaq 84:16
Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa
Verse 17 — Surah Al-Inshiqaq 84:17
Na kwa usiku na unavyo vikusanya
Verse 18 — Surah Al-Inshiqaq 84:18
Na kwa mwezi unapo pevuka
Verse 19 — Surah Al-Inshiqaq 84:19
Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka
Verse 20 — Surah Al-Inshiqaq 84:20
Basi wana nini hawaamini
Verse 21 — Surah Al-Inshiqaq 84:21
Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu
Verse 22 — Surah Al-Inshiqaq 84:22
Bali walio kufuru wanakanusha tu
Verse 23 — Surah Al-Inshiqaq 84:23
Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria
Verse 24 — Surah Al-Inshiqaq 84:24
Basi wabashirie adhabu chungu
Verse 25 — Surah Al-Inshiqaq 84:25
Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika