Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 85 - Al-Buruj
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Buruj 85:1
Naapa kwa mbingu yenye Buruji
Verse 2 — Surah Al-Buruj 85:2
Na kwa siku iliyo ahidiwa
Verse 3 — Surah Al-Buruj 85:3
Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa
Verse 4 — Surah Al-Buruj 85:4
Wameangamizwa watu wa makhandaki
Verse 5 — Surah Al-Buruj 85:5
Yenye moto wenye kuni nyingi
Verse 6 — Surah Al-Buruj 85:6
Walipo kuwa wamekaa hapo
Verse 7 — Surah Al-Buruj 85:7
Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini
Verse 8 — Surah Al-Buruj 85:8
Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa
Verse 9 — Surah Al-Buruj 85:9
Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu
Verse 10 — Surah Al-Buruj 85:10
Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua
Verse 11 — Surah Al-Buruj 85:11
Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa
Verse 12 — Surah Al-Buruj 85:12
Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali
Verse 13 — Surah Al-Buruj 85:13
Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena
Verse 14 — Surah Al-Buruj 85:14
Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi
Verse 15 — Surah Al-Buruj 85:15
Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu
Verse 16 — Surah Al-Buruj 85:16
Atendaye ayatakayo
Verse 17 — Surah Al-Buruj 85:17
Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi
Verse 18 — Surah Al-Buruj 85:18
Ya Firauni na Thamudi
Verse 19 — Surah Al-Buruj 85:19
Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha
Verse 20 — Surah Al-Buruj 85:20
Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka
Verse 21 — Surah Al-Buruj 85:21
Bali hii ni Qur'ani tukufu
Verse 22 — Surah Al-Buruj 85:22
Katika Ubao Ulio Hifadhiwa