Back to Languages

Swahili - Chapter 27 - An-Naml

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah An-Naml 27:1

T'aa Siin. (T'. S.), Hizi ni Aya za Qur'ani na Kitabu kinacho bainisha

Verse 2 — Surah An-Naml 27:2

Uwongofu na bishara kwa Waumini

Verse 3 — Surah An-Naml 27:3

Ambao wanashika Sala, na wanatoa Zaka, na Akhera wana yakini nayo

Verse 4 — Surah An-Naml 27:4

Kwa hakika wale wasio iamini Akhera tumewapambia vitendo vyao, kwa hivyo wanatangatanga ovyo

Verse 5 — Surah An-Naml 27:5

Hao ndio watapata adhabu mbaya kabisa, na hao katika Akhera ndio watapata khasara zaidi

Verse 6 — Surah An-Naml 27:6

Na hakika wewe unafundishwa Qur'ani inayo tokana kwake Mwenye hikima Mwenye kujua

Verse 7 — Surah An-Naml 27:7

(Kumbuka) Musa alipo waambia ahali zake: Hakika nimeona moto, nitakwenda nikuleteeni khabari, au nitakuleteeni kijinga kinacho waka ili mpate kuota moto

Verse 8 — Surah An-Naml 27:8

Basi alipo fika ilinadiwa: Amebarikiwa aliomo katika moto huu na walioko pembezoni mwake. Na ametakasika Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 9 — Surah An-Naml 27:9

Ewe Musa! Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima

Verse 10 — Surah An-Naml 27:10

Na itupe fimbo yako! Alipo iona ikitikisika kama nyoka, aligeuka nyuma wala hakungoja. Ewe Musa! Usikhofu! Hakika hawakhofu mbele yangu Mitume

Verse 11 — Surah An-Naml 27:11

Lakini aliye dhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya ubaya, basi Mimi ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu

Verse 12 — Surah An-Naml 27:12

Na ingiza mkono wako katika mfuko wako, utatoka mweupe bila ya maradhi. Ni katika Ishara tisa za kumpelekea Firauni na kaumu yake. Hakika hao walikuwa watu waovu

Verse 13 — Surah An-Naml 27:13

Basi zilipo wafikia Ishara zetu hizo zenye kuonyesha, wakasema: Huu ni uchawi dhaahiri

Verse 14 — Surah An-Naml 27:14

Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa mafisadi

Verse 15 — Surah An-Naml 27:15

Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi, Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye tufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini

Verse 16 — Surah An-Naml 27:16

Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhaahiri

Verse 17 — Surah An-Naml 27:17

Na alikusanyiwa Sulaiman majeshi yake ya majini, na watu, na ndege; nayo yakapangwa kwa nidhamu

Verse 18 — Surah An-Naml 27:18

Mpaka walipo fika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Sulaiman na majeshi yake bila ya wao kutambua

Verse 19 — Surah An-Naml 27:19

Basi (Sulaiman) akatabasamu akacheka kwa neno hili, na akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema

Verse 20 — Surah An-Naml 27:20

Na akawakagua ndege, na akasema: Imekuwaje, mbona simwoni Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walio ghibu

Verse 21 — Surah An-Naml 27:21

Kwa yakini nitamuadhibu kwa adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja ya kutosha

Verse 22 — Surah An-Naml 27:22

Basi (Hud-hud) akakaa si mbali na akasema: Nimegundua usilo gundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea khabari za yakini

Verse 23 — Surah An-Naml 27:23

Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa

Verse 24 — Surah An-Naml 27:24

Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na Shet'ani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia Njia. Kwa hivyo hawakuongoka

Verse 25 — Surah An-Naml 27:25

Na hawamsujudii Mwenyezi Mungu ambaye huyatoa yaliyo fichikana katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza

Verse 26 — Surah An-Naml 27:26

Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi tukufu

Verse 27 — Surah An-Naml 27:27

Akasema (Sulaiman): Tutatazama umesema kweli au wewe ni miongoni mwa waongo

Verse 28 — Surah An-Naml 27:28

Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha waache na utazame watarejesha nini

Verse 29 — Surah An-Naml 27:29

(Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu

Verse 30 — Surah An-Naml 27:30

Imetoka kwa Sulaiman nayo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

Verse 31 — Surah An-Naml 27:31

Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri

Verse 32 — Surah An-Naml 27:32

Akasema: Enyi wahishimiwa! Nipeni shauri katika jambo langu hili, kwani mimi sikati shauri yoyote mpaka mhudhurie

Verse 33 — Surah An-Naml 27:33

Wakasema: Sisi ni wenye nguvu na wakali kwa vita; na amri iko kwako, basi tazama ni nini unaamrisha

Verse 34 — Surah An-Naml 27:34

Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo

Verse 35 — Surah An-Naml 27:35

Lakini mimi nitawapelekea zawadi, nami nitangoja watakayo rudi nayo wajumbe

Verse 36 — Surah An-Naml 27:36

Basi alipo fika (mjumbe) kwa Sulaiman, alisema (Sulaiman): Hivyo ndio nyinyi mnanisaidia kwa mali? Aliyo nipa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko aliyo kupeni nyinyi. Lakini nyinyi mnafurahia hii zawadi yenu

Verse 37 — Surah An-Naml 27:37

Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasio yaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge

Verse 38 — Surah An-Naml 27:38

Akasema: Enyi wahishimiwa! Ni nani kati yenu atakaye niletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia nao wamekwisha salimu amri

Verse 39 — Surah An-Naml 27:39

Akasema: Afriti, katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako hapo. Na mimi kwa hakika nina nguvu na muaminifu

Verse 40 — Surah An-Naml 27:40

Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu

Verse 41 — Surah An-Naml 27:41

Akasema: Mgeuzieni kiti chake cha enzi hiki, tuone ataongoka, au atakuwa miongoni mwa wasio ongoka

Verse 42 — Surah An-Naml 27:42

Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu

Verse 43 — Surah An-Naml 27:43

Na yale aliyo kuwa akiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yalimzuilia. Hakika yeye (Malkia) alikuwa katika kaumu ya makafiri

Verse 44 — Surah An-Naml 27:44

Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 45 — Surah An-Naml 27:45

Na kwa kina Thamud tulimtuma ndugu yao Saleh kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu. Basi wakawa makundi mawili yanayo gombana

Verse 46 — Surah An-Naml 27:46

Akasema: Enyi watu wangu! Kwa nini mnauhimiza uwovu kabla ya wema? Kwa nini hamuombi msamaha kwa Mwenyezi Mungu ili mrehemewe

Verse 47 — Surah An-Naml 27:47

Wakasema: Tuna kisirani nawe na wale walio pamoja nawe. Yeye akasema: Uaguzi wa ukorofi wenu uko kwa Mwenyezi Mungu; lakini nyinyi ni watu mnao jaribiwa

Verse 48 — Surah An-Naml 27:48

Na walikuwamo mjini watu tisa wakifanya ufisadi katika nchi wala hawafanyi la maslaha

Verse 49 — Surah An-Naml 27:49

Wakasema: Apishaneni kwa Mwenyezi Mungu tutamshambulia usiku yeye na ahali zake; kisha tutamwambia mrithi wake: Sisi hatukuona maangamizo ya watu wake, na sisi bila ya shaka tunasema kweli

Verse 50 — Surah An-Naml 27:50

Basi wakapanga mipango yao, na Sisi tukapanga mipango yetu, na wao hawatambui

Verse 51 — Surah An-Naml 27:51

Basi angalia ulivyo kuwa mwisho wa mipango yao, ya kwamba tuliwaangamiza wao pamoja na watu wao wote

Verse 52 — Surah An-Naml 27:52

Basi hizo nyumba zao ni tupu kwa sababu ya walivyo dhulumu. Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara kwa watu wanao jua

Verse 53 — Surah An-Naml 27:53

Na tukawaokoa wale walio amini na walio kuwa wanamchamngu

Verse 54 — Surah An-Naml 27:54

Na Lut'i alipo waambia watu wake: Je! Mnafanya uchafu nanyi mnaona

Verse 55 — Surah An-Naml 27:55

Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio badala ya wanawake? Hakika nyinyi ni watu mnao fanya ujinga kabisa

Verse 56 — Surah An-Naml 27:56

Basi haikuwa jawabu ya watu wake ila ni kusema: Wafukuzeni wafwasi wa Lut'i katika mji wenu. Hao ni watu wanao jitia usafi

Verse 57 — Surah An-Naml 27:57

Basi tukamwokoa yeye na ahali zake, isipo kuwa mkewe; tukamkadiria katika walio baki nyuma

Verse 58 — Surah An-Naml 27:58

Na tukawanyeshea mvua. Ni ovu kweli kweli hiyo mvua ya walio kwisha onywa

Verse 59 — Surah An-Naml 27:59

Sema: Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu! Na amani ishuke juu ya waja wake alio wateuwa. Je! Mwenyezi Mungu ni bora, au wale wanao washirikisha naye

Verse 60 — Surah An-Naml 27:60

AU NANI yule aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni watu walio potoka

Verse 61 — Surah An-Naml 27:61

Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui

Verse 62 — Surah An-Naml 27:62

Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia

Verse 63 — Surah An-Naml 27:63

Au nani yule anaye kuongoeni katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya wanao washirikisha naye

Verse 64 — Surah An-Naml 27:64

Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli

Verse 65 — Surah An-Naml 27:65

Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao hawajui lini watafufuliwa

Verse 66 — Surah An-Naml 27:66

Kwani huo ujuzi wao umefikilia kuijua Akhera? Bali wao wamo katika shaka nayo tu, bali wao ni vipofu nayo

Verse 67 — Surah An-Naml 27:67

Na wakasema walio kufuru: Tutapo kuwa mchanga, sisi na baba zetu, hivyo kweli tutakuja tolewa

Verse 68 — Surah An-Naml 27:68

Haya haya tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni hadithi za uwongo za watu wa kale

Verse 69 — Surah An-Naml 27:69

Sema: Nendeni katika ardhi, na tazameni ulikuwaje mwisho wa wakosefu

Verse 70 — Surah An-Naml 27:70

Wala usiwahuzunukie wala usiwe katika dhiki kwa sababu ya hila zao wanazo zifanya

Verse 71 — Surah An-Naml 27:71

Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa mnasema kweli

Verse 72 — Surah An-Naml 27:72

Sema: Asaa ni karibu kukufikieni sehemu ya yale mnayo yahimiza

Verse 73 — Surah An-Naml 27:73

Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye fadhila kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru

Verse 74 — Surah An-Naml 27:74

Na hakika Mola wako Mlezi anayajua yanayo ficha vifua vyao na wanayo yatangaza

Verse 75 — Surah An-Naml 27:75

Na hakuna siri katika mbingu na ardhi ila imo katika Kitabu kinacho bainisha

Verse 76 — Surah An-Naml 27:76

Hakika Qur'ani hii inawasimulia Wana wa Israili mengi wanayo khitalifiana nayo

Verse 77 — Surah An-Naml 27:77

Nayo hakika ni Uwongofu na Rehema kwa Waumini

Verse 78 — Surah An-Naml 27:78

Hakika Mola wako Mlezi atawahukumu kwa hukumu yake, naye ni Mwenye nguvu Mjuzi

Verse 79 — Surah An-Naml 27:79

Basi mtegemee Mweneyezi Mungu; hakika wewe uko juu ya Haki iliyo wazi

Verse 80 — Surah An-Naml 27:80

Kwa hakika wewe huwezi kuwafanya maiti wasikie, wala kuwafanya viziwi wasikie wito, wanapo kwisha geuka kwenda zao

Verse 81 — Surah An-Naml 27:81

Wala huwezi kuwaongoa vipofu waache upotovu wao. Huwezi kuwafanya wasikie isipo kuwa wenye kuziamini Ishara zetu; na hao ndio wat'iifu

Verse 82 — Surah An-Naml 27:82

Na itapo waangukia kauli juu yao, tutawatolea mnyama katika ardhi atakaye wasemeza, ya kuwa watu walikuwa hawana na yakini na Ishara zetu

Verse 83 — Surah An-Naml 27:83

Na Siku tutapo kusanya kutoka kila umma kundi katika wanao kadhibisha Ishara zetu, nao watagawanywa mafungu mafungu

Verse 84 — Surah An-Naml 27:84

Hata watakapo fika, atasema (Mwenyezi Mungu): Je! Nyinyi si mlizikanusha Ishara zangu pasipo kuzijua vyema? Au mlikuwa mkifanya nini

Verse 85 — Surah An-Naml 27:85

Na kauli itawaangukia juu yao kwa vile walivyo dhulumu. Basi hao hawatasema lolote

Verse 86 — Surah An-Naml 27:86

Je! Hawaoni kwamba sisi tumeufanya usiku ili watulie, na mchana wa kuangaza. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao amini

Verse 87 — Surah An-Naml 27:87

Na Siku litapo pulizwa baragumu, watahangaika waliomo mbinguni na katika ardhi, ila amtakaye Mwenyezi Mungu. Na wote watamfikia nao ni wanyonge

Verse 88 — Surah An-Naml 27:88

Na unaiona milima unaidhunia imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu. Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu. Hakika Yeye anazo khabari za yote myatendayo

Verse 89 — Surah An-Naml 27:89

Watakao kuja na mema, watapata bora kuliko hayo. Nao watasalimika na mahangaiko ya Siku hiyo

Verse 90 — Surah An-Naml 27:90

Na watakao kuja na uovu, basi zitasunukishwa nyuso zao Motoni. Je! Kwani mnalipwa isipo kuwa mliyo kuwa mkiyatenda

Verse 91 — Surah An-Naml 27:91

Ama mimi nimeamrishwa nimuabudu Mola Mlezi wa mji huu aliye ufanya ni mtakatifu; na ni vyake Yeye tu vitu vyote. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu, wenye kunyenyekea

Verse 92 — Surah An-Naml 27:92

Na niisome Qur'ani. Na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi yake; na aliye potea - basi sema: Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji

Verse 93 — Surah An-Naml 27:93

Na sema: Alhamdu Lillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Yeye atakuonyesheni Ishara zake, na mtazijua. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika na myatendayo