Back to Languages

Swahili - Chapter 26 - Ash-Shuara

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah Ash-Shuara 26:1

T'aa Siin Miim. (T'. S. M)

Verse 2 — Surah Ash-Shuara 26:2

Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha

Verse 3 — Surah Ash-Shuara 26:3

Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini

Verse 4 — Surah Ash-Shuara 26:4

Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao

Verse 5 — Surah Ash-Shuara 26:5

Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga nao

Verse 6 — Surah Ash-Shuara 26:6

Kwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia khabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha

Verse 7 — Surah Ash-Shuara 26:7

Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri

Verse 8 — Surah Ash-Shuara 26:8

Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini

Verse 9 — Surah Ash-Shuara 26:9

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu

Verse 10 — Surah Ash-Shuara 26:10

Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fika kwa watu madhaalimu

Verse 11 — Surah Ash-Shuara 26:11

Watu wa Firauni. Hawaogopi

Verse 12 — Surah Ash-Shuara 26:12

Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe

Verse 13 — Surah Ash-Shuara 26:13

Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun

Verse 14 — Surah Ash-Shuara 26:14

Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa

Verse 15 — Surah Ash-Shuara 26:15

Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza

Verse 16 — Surah Ash-Shuara 26:16

Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 17 — Surah Ash-Shuara 26:17

Waachilie Wana wa Israili wende nasi

Verse 18 — Surah Ash-Shuara 26:18

(Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi

Verse 19 — Surah Ash-Shuara 26:19

Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani

Verse 20 — Surah Ash-Shuara 26:20

(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa wale walio potea

Verse 21 — Surah Ash-Shuara 26:21

Basi nikakukimbieni nilipo kuogopeni, tena Mola wangu Mlezi akanitunukia hukumu, na akanijaalia niwe miongoni mwa Mitume

Verse 22 — Surah Ash-Shuara 26:22

Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili

Verse 23 — Surah Ash-Shuara 26:23

Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 24 — Surah Ash-Shuara 26:24

Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini

Verse 25 — Surah Ash-Shuara 26:25

(Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi

Verse 26 — Surah Ash-Shuara 26:26

(Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza

Verse 27 — Surah Ash-Shuara 26:27

(Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu

Verse 28 — Surah Ash-Shuara 26:28

(Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini

Verse 29 — Surah Ash-Shuara 26:29

(Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani

Verse 30 — Surah Ash-Shuara 26:30

Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi

Verse 31 — Surah Ash-Shuara 26:31

Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli

Verse 32 — Surah Ash-Shuara 26:32

Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri

Verse 33 — Surah Ash-Shuara 26:33

Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao

Verse 34 — Surah Ash-Shuara 26:34

(Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu

Verse 35 — Surah Ash-Shuara 26:35

Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani

Verse 36 — Surah Ash-Shuara 26:36

Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo

Verse 37 — Surah Ash-Shuara 26:37

Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu

Verse 38 — Surah Ash-Shuara 26:38

Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu

Verse 39 — Surah Ash-Shuara 26:39

Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika

Verse 40 — Surah Ash-Shuara 26:40

Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda

Verse 41 — Surah Ash-Shuara 26:41

Basi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda

Verse 42 — Surah Ash-Shuara 26:42

Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele

Verse 43 — Surah Ash-Shuara 26:43

Musa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa

Verse 44 — Surah Ash-Shuara 26:44

Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda

Verse 45 — Surah Ash-Shuara 26:45

Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua

Verse 46 — Surah Ash-Shuara 26:46

Hapo wachawi walipinduka wakasujudu

Verse 47 — Surah Ash-Shuara 26:47

Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 48 — Surah Ash-Shuara 26:48

Mola Mlezi wa Musa na Harun

Verse 49 — Surah Ash-Shuara 26:49

(Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakubandikeni misalabani nyote

Verse 50 — Surah Ash-Shuara 26:50

Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi

Verse 51 — Surah Ash-Shuara 26:51

Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini

Verse 52 — Surah Ash-Shuara 26:52

Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa

Verse 53 — Surah Ash-Shuara 26:53

Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo

Verse 54 — Surah Ash-Shuara 26:54

(Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo

Verse 55 — Surah Ash-Shuara 26:55

Verse 56 — Surah Ash-Shuara 26:56

Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari

Verse 57 — Surah Ash-Shuara 26:57

Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem

Verse 58 — Surah Ash-Shuara 26:58

Na makhazina, na vyeo vya hishima

Verse 59 — Surah Ash-Shuara 26:59

Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili

Verse 60 — Surah Ash-Shuara 26:60

Basi wakawafuata lilipo chomoza jua

Verse 61 — Surah Ash-Shuara 26:61

Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana

Verse 62 — Surah Ash-Shuara 26:62

(Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa

Verse 63 — Surah Ash-Shuara 26:63

Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa

Verse 64 — Surah Ash-Shuara 26:64

Na tukawajongeza hapo wale wengine

Verse 65 — Surah Ash-Shuara 26:65

Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote

Verse 66 — Surah Ash-Shuara 26:66

Kisha tukawazamisha hao wengine

Verse 67 — Surah Ash-Shuara 26:67

Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini

Verse 68 — Surah Ash-Shuara 26:68

Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu

Verse 69 — Surah Ash-Shuara 26:69

Na wasomee khabari za Ibrahim

Verse 70 — Surah Ash-Shuara 26:70

Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini

Verse 71 — Surah Ash-Shuara 26:71

Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea

Verse 72 — Surah Ash-Shuara 26:72

Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita

Verse 73 — Surah Ash-Shuara 26:73

Au yanakufaeni, au yanakudhuruni

Verse 74 — Surah Ash-Shuara 26:74

Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo

Verse 75 — Surah Ash-Shuara 26:75

Je! Mmewaona hawa mnao waabudu

Verse 76 — Surah Ash-Shuara 26:76

Nyinyi na baba zenu wa zamani

Verse 77 — Surah Ash-Shuara 26:77

Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 78 — Surah Ash-Shuara 26:78

Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa

Verse 79 — Surah Ash-Shuara 26:79

Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha

Verse 80 — Surah Ash-Shuara 26:80

Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha

Verse 81 — Surah Ash-Shuara 26:81

Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha

Verse 82 — Surah Ash-Shuara 26:82

Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo

Verse 83 — Surah Ash-Shuara 26:83

Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema

Verse 84 — Surah Ash-Shuara 26:84

Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye

Verse 85 — Surah Ash-Shuara 26:85

Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema

Verse 86 — Surah Ash-Shuara 26:86

Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu

Verse 87 — Surah Ash-Shuara 26:87

Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa

Verse 88 — Surah Ash-Shuara 26:88

Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana

Verse 89 — Surah Ash-Shuara 26:89

Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi

Verse 90 — Surah Ash-Shuara 26:90

Na Pepo itasogezwa kwa wachamngu

Verse 91 — Surah Ash-Shuara 26:91

Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu

Verse 92 — Surah Ash-Shuara 26:92

Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu

Verse 93 — Surah Ash-Shuara 26:93

Badala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia wenyewe

Verse 94 — Surah Ash-Shuara 26:94

Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu

Verse 95 — Surah Ash-Shuara 26:95

Na majeshi ya Ibilisi yote

Verse 96 — Surah Ash-Shuara 26:96

Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo

Verse 97 — Surah Ash-Shuara 26:97

Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri

Verse 98 — Surah Ash-Shuara 26:98

Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 99 — Surah Ash-Shuara 26:99

Na hawakutupoteza ila wale wakosefu

Verse 100 — Surah Ash-Shuara 26:100

Verse 101 — Surah Ash-Shuara 26:101

Verse 102 — Surah Ash-Shuara 26:102

Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini

Verse 103 — Surah Ash-Shuara 26:103

Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini

Verse 104 — Surah Ash-Shuara 26:104

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu

Verse 105 — Surah Ash-Shuara 26:105

Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume

Verse 106 — Surah Ash-Shuara 26:106

Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu

Verse 107 — Surah Ash-Shuara 26:107

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu

Verse 108 — Surah Ash-Shuara 26:108

Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi

Verse 109 — Surah Ash-Shuara 26:109

Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 110 — Surah Ash-Shuara 26:110

Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi

Verse 111 — Surah Ash-Shuara 26:111

Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini

Verse 112 — Surah Ash-Shuara 26:112

Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya

Verse 113 — Surah Ash-Shuara 26:113

Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua

Verse 114 — Surah Ash-Shuara 26:114

Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini

Verse 115 — Surah Ash-Shuara 26:115

Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri

Verse 116 — Surah Ash-Shuara 26:116

Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe

Verse 117 — Surah Ash-Shuara 26:117

Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha

Verse 118 — Surah Ash-Shuara 26:118

Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini

Verse 119 — Surah Ash-Shuara 26:119

Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni

Verse 120 — Surah Ash-Shuara 26:120

Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia

Verse 121 — Surah Ash-Shuara 26:121

Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao walio kuwa Waumini

Verse 122 — Surah Ash-Shuara 26:122

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu

Verse 123 — Surah Ash-Shuara 26:123

Kina A'd waliwakanusha Mitume

Verse 124 — Surah Ash-Shuara 26:124

Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu

Verse 125 — Surah Ash-Shuara 26:125

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu

Verse 126 — Surah Ash-Shuara 26:126

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi

Verse 127 — Surah Ash-Shuara 26:127

Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 128 — Surah Ash-Shuara 26:128

Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi

Verse 129 — Surah Ash-Shuara 26:129

Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele

Verse 130 — Surah Ash-Shuara 26:130

Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari

Verse 131 — Surah Ash-Shuara 26:131

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini

Verse 132 — Surah Ash-Shuara 26:132

Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua

Verse 133 — Surah Ash-Shuara 26:133

Amekupeni wanyama wa kufuga na wana

Verse 134 — Surah Ash-Shuara 26:134

Na mabustani na chemchem

Verse 135 — Surah Ash-Shuara 26:135

Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa

Verse 136 — Surah Ash-Shuara 26:136

Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha

Verse 137 — Surah Ash-Shuara 26:137

Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani

Verse 138 — Surah Ash-Shuara 26:138

Wala sisi hatutaadhibiwa

Verse 139 — Surah Ash-Shuara 26:139

Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini

Verse 140 — Surah Ash-Shuara 26:140

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu

Verse 141 — Surah Ash-Shuara 26:141

Kina Thamud waliwakanusha Mitume

Verse 142 — Surah Ash-Shuara 26:142

Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchimngu

Verse 143 — Surah Ash-Shuara 26:143

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu

Verse 144 — Surah Ash-Shuara 26:144

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini

Verse 145 — Surah Ash-Shuara 26:145

Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 146 — Surah Ash-Shuara 26:146

Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa

Verse 147 — Surah Ash-Shuara 26:147

Katika mabustani, na chemchem

Verse 148 — Surah Ash-Shuara 26:148

Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva

Verse 149 — Surah Ash-Shuara 26:149

Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi

Verse 150 — Surah Ash-Shuara 26:150

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi

Verse 151 — Surah Ash-Shuara 26:151

Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka

Verse 152 — Surah Ash-Shuara 26:152

Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi

Verse 153 — Surah Ash-Shuara 26:153

Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa

Verse 154 — Surah Ash-Shuara 26:154

Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli

Verse 155 — Surah Ash-Shuara 26:155

Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu

Verse 156 — Surah Ash-Shuara 26:156

Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa

Verse 157 — Surah Ash-Shuara 26:157

Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta

Verse 158 — Surah Ash-Shuara 26:158

Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini

Verse 159 — Surah Ash-Shuara 26:159

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu

Verse 160 — Surah Ash-Shuara 26:160

Watu wa Lut'i waliwakanusha Mitume

Verse 161 — Surah Ash-Shuara 26:161

Alipo waambia ndugu yao, Lut'i: Je! Hamumchimngu

Verse 162 — Surah Ash-Shuara 26:162

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu

Verse 163 — Surah Ash-Shuara 26:163

Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi

Verse 164 — Surah Ash-Shuara 26:164

Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 165 — Surah Ash-Shuara 26:165

Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume

Verse 166 — Surah Ash-Shuara 26:166

Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka

Verse 167 — Surah Ash-Shuara 26:167

Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji

Verse 168 — Surah Ash-Shuara 26:168

Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu

Verse 169 — Surah Ash-Shuara 26:169

Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo

Verse 170 — Surah Ash-Shuara 26:170

Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote

Verse 171 — Surah Ash-Shuara 26:171

Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma

Verse 172 — Surah Ash-Shuara 26:172

Kisha tukawaangamiza wale wengine

Verse 173 — Surah Ash-Shuara 26:173

Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa

Verse 174 — Surah Ash-Shuara 26:174

Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini

Verse 175 — Surah Ash-Shuara 26:175

Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu

Verse 176 — Surah Ash-Shuara 26:176

Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume

Verse 177 — Surah Ash-Shuara 26:177

Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu

Verse 178 — Surah Ash-Shuara 26:178

Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu

Verse 179 — Surah Ash-Shuara 26:179

Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi

Verse 180 — Surah Ash-Shuara 26:180

Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 181 — Surah Ash-Shuara 26:181

Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja

Verse 182 — Surah Ash-Shuara 26:182

Na pimeni kwa haki iliyo nyooka

Verse 183 — Surah Ash-Shuara 26:183

Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi

Verse 184 — Surah Ash-Shuara 26:184

Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia

Verse 185 — Surah Ash-Shuara 26:185

Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa

Verse 186 — Surah Ash-Shuara 26:186

Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo

Verse 187 — Surah Ash-Shuara 26:187

Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli

Verse 188 — Surah Ash-Shuara 26:188

Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda

Verse 189 — Surah Ash-Shuara 26:189

Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa

Verse 190 — Surah Ash-Shuara 26:190

Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini

Verse 191 — Surah Ash-Shuara 26:191

Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu

Verse 192 — Surah Ash-Shuara 26:192

Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote

Verse 193 — Surah Ash-Shuara 26:193

Ameuteremsha Roho muaminifu

Verse 194 — Surah Ash-Shuara 26:194

Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji

Verse 195 — Surah Ash-Shuara 26:195

Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi

Verse 196 — Surah Ash-Shuara 26:196

Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale

Verse 197 — Surah Ash-Shuara 26:197

Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili

Verse 198 — Surah Ash-Shuara 26:198

Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu

Verse 199 — Surah Ash-Shuara 26:199

Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini

Verse 200 — Surah Ash-Shuara 26:200

Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu

Verse 201 — Surah Ash-Shuara 26:201

Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu

Verse 202 — Surah Ash-Shuara 26:202

Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari

Verse 203 — Surah Ash-Shuara 26:203

Na watasema: Je, tutapewa muhula

Verse 204 — Surah Ash-Shuara 26:204

Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu

Verse 205 — Surah Ash-Shuara 26:205

Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka

Verse 206 — Surah Ash-Shuara 26:206

Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa

Verse 207 — Surah Ash-Shuara 26:207

Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa

Verse 208 — Surah Ash-Shuara 26:208

Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji

Verse 209 — Surah Ash-Shuara 26:209

Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu

Verse 210 — Surah Ash-Shuara 26:210

Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo

Verse 211 — Surah Ash-Shuara 26:211

Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi

Verse 212 — Surah Ash-Shuara 26:212

Hakika hao wametengwa na kusikia

Verse 213 — Surah Ash-Shuara 26:213

Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa

Verse 214 — Surah Ash-Shuara 26:214

Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe

Verse 215 — Surah Ash-Shuara 26:215

Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini

Verse 216 — Surah Ash-Shuara 26:216

Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda

Verse 217 — Surah Ash-Shuara 26:217

Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu

Verse 218 — Surah Ash-Shuara 26:218

Ambaye anakuona unapo simama

Verse 219 — Surah Ash-Shuara 26:219

Na mageuko yako kati ya wanao sujudu

Verse 220 — Surah Ash-Shuara 26:220

Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua

Verse 221 — Surah Ash-Shuara 26:221

Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani

Verse 222 — Surah Ash-Shuara 26:222

Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi

Verse 223 — Surah Ash-Shuara 26:223

Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo

Verse 224 — Surah Ash-Shuara 26:224

Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata

Verse 225 — Surah Ash-Shuara 26:225

Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde

Verse 226 — Surah Ash-Shuara 26:226

Na kwamba wao husema wasiyo yatenda

Verse 227 — Surah Ash-Shuara 26:227

Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka