Back to Languages

Swahili - Chapter 52 - At-Tur

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah At-Tur 52:1

Naapa kwa mlima wa T'ur

Verse 2 — Surah At-Tur 52:2

Na Kitabu kilicho andikwa

Verse 3 — Surah At-Tur 52:3

Katika ngozi iliyo kunjuliwa

Verse 4 — Surah At-Tur 52:4

Na kwa Nyumba iliyo jengwa

Verse 5 — Surah At-Tur 52:5

Na kwa dari iliyo nyanyuliwa

Verse 6 — Surah At-Tur 52:6

Na kwa bahari iliyo jazwa

Verse 7 — Surah At-Tur 52:7

Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea

Verse 8 — Surah At-Tur 52:8

Verse 9 — Surah At-Tur 52:9

Siku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso

Verse 10 — Surah At-Tur 52:10

Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa

Verse 11 — Surah At-Tur 52:11

Basi ole wao siku hiyo hao wanao kadhibisha

Verse 12 — Surah At-Tur 52:12

Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi

Verse 13 — Surah At-Tur 52:13

Siku watapo sukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu

Verse 14 — Surah At-Tur 52:14

(Waambiwe): Huu ndio ule Moto mlio kuwa mkiukanusha

Verse 15 — Surah At-Tur 52:15

Je! Huu ni uchawi, au hamwoni tu

Verse 16 — Surah At-Tur 52:16

Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyo kuwa mkiyatenda

Verse 17 — Surah At-Tur 52:17

Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na neema

Verse 18 — Surah At-Tur 52:18

Wakifurahi kwa yale aliyo wapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni

Verse 19 — Surah At-Tur 52:19

Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyatenda

Verse 20 — Surah At-Tur 52:20

Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza mahuru-l-aini

Verse 21 — Surah At-Tur 52:21

Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma

Verse 22 — Surah At-Tur 52:22

Na tutawapa matunda, na nyama kama watavyo penda

Verse 23 — Surah At-Tur 52:23

Watapeana humo bilauri zisio na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi

Verse 24 — Surah At-Tur 52:24

Iwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza

Verse 25 — Surah At-Tur 52:25

Wataelekeana wakiulizana

Verse 26 — Surah At-Tur 52:26

Waseme: Tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa

Verse 27 — Surah At-Tur 52:27

Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda na adhabu ya upepo wa Moto

Verse 28 — Surah At-Tur 52:28

Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwenye kurehemu

Verse 29 — Surah At-Tur 52:29

Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu

Verse 30 — Surah At-Tur 52:30

Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari

Verse 31 — Surah At-Tur 52:31

Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia

Verse 32 — Surah At-Tur 52:32

Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu

Verse 33 — Surah At-Tur 52:33

Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini

Verse 34 — Surah At-Tur 52:34

Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli

Verse 35 — Surah At-Tur 52:35

Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji

Verse 36 — Surah At-Tur 52:36

Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini

Verse 37 — Surah At-Tur 52:37

Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka

Verse 38 — Surah At-Tur 52:38

Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi

Verse 39 — Surah At-Tur 52:39

Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana

Verse 40 — Surah At-Tur 52:40

Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama

Verse 41 — Surah At-Tur 52:41

Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika

Verse 42 — Surah At-Tur 52:42

Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka

Verse 43 — Surah At-Tur 52:43

Au wanae mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametaksika Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye

Verse 44 — Surah At-Tur 52:44

Na hata wange ona pande linatoka mbinguni linaanguka wange sema: Ni mawingu yaliyo bebana

Verse 45 — Surah At-Tur 52:45

Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapo hilikishwa

Verse 46 — Surah At-Tur 52:46

Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa

Verse 47 — Surah At-Tur 52:47

Na hakika walio dhulumu watapata adhabu nyengine isiyo kuwa hii, lakini wengi wao hawajui

Verse 48 — Surah At-Tur 52:48

Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama

Verse 49 — Surah At-Tur 52:49

Na usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota