Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 56 - Al-Waqiah
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Waqiah 56:1
Litakapo tukia hilo Tukio
Verse 2 — Surah Al-Waqiah 56:2
Hapana cha kukanusha kutukia kwake
Verse 3 — Surah Al-Waqiah 56:3
Literemshalo linyanyualo
Verse 4 — Surah Al-Waqiah 56:4
Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso
Verse 5 — Surah Al-Waqiah 56:5
Na milima itapo sagwasagwa
Verse 6 — Surah Al-Waqiah 56:6
Iwe mavumbi yanayo peperushwa
Verse 7 — Surah Al-Waqiah 56:7
Na nyinyi mtakuwa namna tatu
Verse 8 — Surah Al-Waqiah 56:8
Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani
Verse 9 — Surah Al-Waqiah 56:9
Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni
Verse 10 — Surah Al-Waqiah 56:10
Na wa mbele watakuwa mbele
Verse 11 — Surah Al-Waqiah 56:11
Hao ndio watakao karibishwa
Verse 12 — Surah Al-Waqiah 56:12
Katika Bustani zenye neema
Verse 13 — Surah Al-Waqiah 56:13
Fungu kubwa katika wa mwanzo
Verse 14 — Surah Al-Waqiah 56:14
Na wachache katika wa mwisho
Verse 15 — Surah Al-Waqiah 56:15
Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa
Verse 16 — Surah Al-Waqiah 56:16
Wakiviegemea wakielekeana
Verse 17 — Surah Al-Waqiah 56:17
Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele
Verse 18 — Surah Al-Waqiah 56:18
Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi
Verse 19 — Surah Al-Waqiah 56:19
Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa
Verse 20 — Surah Al-Waqiah 56:20
Na matunda wayapendayo
Verse 21 — Surah Al-Waqiah 56:21
Na nyama za ndege kama wanavyo tamani
Verse 22 — Surah Al-Waqiah 56:22
Na Mahurulaini
Verse 23 — Surah Al-Waqiah 56:23
Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa
Verse 24 — Surah Al-Waqiah 56:24
Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda
Verse 25 — Surah Al-Waqiah 56:25
Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi
Verse 26 — Surah Al-Waqiah 56:26
Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama
Verse 27 — Surah Al-Waqiah 56:27
Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani
Verse 28 — Surah Al-Waqiah 56:28
Katika mikunazi isiyo na miba
Verse 29 — Surah Al-Waqiah 56:29
Na migomba iliyo pangiliwa
Verse 30 — Surah Al-Waqiah 56:30
Na kivuli kilicho tanda
Verse 31 — Surah Al-Waqiah 56:31
Na maji yanayo miminika
Verse 32 — Surah Al-Waqiah 56:32
Na matunda mengi
Verse 33 — Surah Al-Waqiah 56:33
Hayatindikii wala hayakatazwi
Verse 34 — Surah Al-Waqiah 56:34
Na matandiko yaliyo nyanyuliwa
Verse 35 — Surah Al-Waqiah 56:35
Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya
Verse 36 — Surah Al-Waqiah 56:36
Na tutawafanya vijana
Verse 37 — Surah Al-Waqiah 56:37
Wanapendana na waume zao, hirimu moja
Verse 38 — Surah Al-Waqiah 56:38
Kwa ajili ya watu wa kuliani
Verse 39 — Surah Al-Waqiah 56:39
Fungu kubwa katika wa mwanzo
Verse 40 — Surah Al-Waqiah 56:40
Na fungu kubwa katika wa mwisho
Verse 41 — Surah Al-Waqiah 56:41
Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni
Verse 42 — Surah Al-Waqiah 56:42
Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka
Verse 43 — Surah Al-Waqiah 56:43
Na kivuli cha moshi mweusi
Verse 44 — Surah Al-Waqiah 56:44
Si cha kuburudisha wala kustarehesha
Verse 45 — Surah Al-Waqiah 56:45
Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa
Verse 46 — Surah Al-Waqiah 56:46
Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa
Verse 47 — Surah Al-Waqiah 56:47
Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa
Verse 48 — Surah Al-Waqiah 56:48
Au baba zetu wa zamani
Verse 49 — Surah Al-Waqiah 56:49
Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho
Verse 50 — Surah Al-Waqiah 56:50
Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu
Verse 51 — Surah Al-Waqiah 56:51
Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha
Verse 52 — Surah Al-Waqiah 56:52
Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu
Verse 53 — Surah Al-Waqiah 56:53
Na kwa mti huo mtajaza matumbo
Verse 54 — Surah Al-Waqiah 56:54
Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka
Verse 55 — Surah Al-Waqiah 56:55
Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu
Verse 56 — Surah Al-Waqiah 56:56
Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo
Verse 57 — Surah Al-Waqiah 56:57
Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki
Verse 58 — Surah Al-Waqiah 56:58
Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza
Verse 59 — Surah Al-Waqiah 56:59
Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji
Verse 60 — Surah Al-Waqiah 56:60
Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi
Verse 61 — Surah Al-Waqiah 56:61
Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua
Verse 62 — Surah Al-Waqiah 56:62
Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki
Verse 63 — Surah Al-Waqiah 56:63
Je! Mnaona makulima mnayo yapanda
Verse 64 — Surah Al-Waqiah 56:64
Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha
Verse 65 — Surah Al-Waqiah 56:65
Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu
Verse 66 — Surah Al-Waqiah 56:66
Mkisema: Hakika sisi tumegharimika
Verse 67 — Surah Al-Waqiah 56:67
Bali sisi tumenyimwa
Verse 68 — Surah Al-Waqiah 56:68
Je! Mnayaona maji mnayo yanywa
Verse 69 — Surah Al-Waqiah 56:69
Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha
Verse 70 — Surah Al-Waqiah 56:70
Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru
Verse 71 — Surah Al-Waqiah 56:71
Je! Mnauona moto mnao uwasha
Verse 72 — Surah Al-Waqiah 56:72
Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji
Verse 73 — Surah Al-Waqiah 56:73
Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani
Verse 74 — Surah Al-Waqiah 56:74
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu
Verse 75 — Surah Al-Waqiah 56:75
Basi naapa kwa maanguko ya nyota
Verse 76 — Surah Al-Waqiah 56:76
Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua
Verse 77 — Surah Al-Waqiah 56:77
Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu
Verse 78 — Surah Al-Waqiah 56:78
Katika Kitabu kilicho hifadhiwa
Verse 79 — Surah Al-Waqiah 56:79
Hapana akigusaye ila walio takaswa
Verse 80 — Surah Al-Waqiah 56:80
Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote
Verse 81 — Surah Al-Waqiah 56:81
Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza
Verse 82 — Surah Al-Waqiah 56:82
Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha
Verse 83 — Surah Al-Waqiah 56:83
Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo
Verse 84 — Surah Al-Waqiah 56:84
Na nyinyi wakati huo mnatazama
Verse 85 — Surah Al-Waqiah 56:85
Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi
Verse 86 — Surah Al-Waqiah 56:86
Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu
Verse 87 — Surah Al-Waqiah 56:87
Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli
Verse 88 — Surah Al-Waqiah 56:88
Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa
Verse 89 — Surah Al-Waqiah 56:89
Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema
Verse 90 — Surah Al-Waqiah 56:90
Na akiwa katika watu wa upande wa kulia
Verse 91 — Surah Al-Waqiah 56:91
Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia
Verse 92 — Surah Al-Waqiah 56:92
Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu
Verse 93 — Surah Al-Waqiah 56:93
Basi karamu yake ni maji yanayo chemka
Verse 94 — Surah Al-Waqiah 56:94
Na kutiwa Motoni
Verse 95 — Surah Al-Waqiah 56:95
Hakika hii ndiyo haki yenye yakini
Verse 96 — Surah Al-Waqiah 56:96
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa