Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 54 - Al-Qamar
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Qamar 54:1
Saa imekaribia, na mwezi umepasuka
Verse 2 — Surah Al-Qamar 54:2
Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea
Verse 3 — Surah Al-Qamar 54:3
Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti
Verse 4 — Surah Al-Qamar 54:4
Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio
Verse 5 — Surah Al-Qamar 54:5
Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu
Verse 6 — Surah Al-Qamar 54:6
Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha
Verse 7 — Surah Al-Qamar 54:7
Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika
Verse 8 — Surah Al-Qamar 54:8
Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu
Verse 9 — Surah Al-Qamar 54:9
Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa
Verse 10 — Surah Al-Qamar 54:10
Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru
Verse 11 — Surah Al-Qamar 54:11
Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika
Verse 12 — Surah Al-Qamar 54:12
Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa
Verse 13 — Surah Al-Qamar 54:13
Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba
Verse 14 — Surah Al-Qamar 54:14
Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa
Verse 15 — Surah Al-Qamar 54:15
Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka
Verse 16 — Surah Al-Qamar 54:16
Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu
Verse 17 — Surah Al-Qamar 54:17
Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka
Verse 18 — Surah Al-Qamar 54:18
Kina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu
Verse 19 — Surah Al-Qamar 54:19
Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo
Verse 20 — Surah Al-Qamar 54:20
Ukiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng'olewa
Verse 21 — Surah Al-Qamar 54:21
Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu
Verse 22 — Surah Al-Qamar 54:22
Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka
Verse 23 — Surah Al-Qamar 54:23
Thamudi waliwakanusha Waonyaji
Verse 24 — Surah Al-Qamar 54:24
Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa
Verse 25 — Surah Al-Qamar 54:25
Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi
Verse 26 — Surah Al-Qamar 54:26
Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi
Verse 27 — Surah Al-Qamar 54:27
Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili
Verse 28 — Surah Al-Qamar 54:28
Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika
Verse 29 — Surah Al-Qamar 54:29
Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja
Verse 30 — Surah Al-Qamar 54:30
Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu
Verse 31 — Surah Al-Qamar 54:31
Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa
Verse 32 — Surah Al-Qamar 54:32
Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye
Verse 33 — Surah Al-Qamar 54:33
Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji
Verse 34 — Surah Al-Qamar 54:34
Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri
Verse 35 — Surah Al-Qamar 54:35
Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru
Verse 36 — Surah Al-Qamar 54:36
Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo
Verse 37 — Surah Al-Qamar 54:37
Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu
Verse 38 — Surah Al-Qamar 54:38
Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea
Verse 39 — Surah Al-Qamar 54:39
Basi onjeni adhabu na maonyo yangu
Verse 40 — Surah Al-Qamar 54:40
Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka
Verse 41 — Surah Al-Qamar 54:41
Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni
Verse 42 — Surah Al-Qamar 54:42
Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza
Verse 43 — Surah Al-Qamar 54:43
Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani
Verse 44 — Surah Al-Qamar 54:44
Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu
Verse 45 — Surah Al-Qamar 54:45
Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma
Verse 46 — Surah Al-Qamar 54:46
Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi
Verse 47 — Surah Al-Qamar 54:47
Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu
Verse 48 — Surah Al-Qamar 54:48
Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu
Verse 49 — Surah Al-Qamar 54:49
Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo
Verse 50 — Surah Al-Qamar 54:50
Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho
Verse 51 — Surah Al-Qamar 54:51
Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka
Verse 52 — Surah Al-Qamar 54:52
Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni
Verse 53 — Surah Al-Qamar 54:53
Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa
Verse 54 — Surah Al-Qamar 54:54
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito
Verse 55 — Surah Al-Qamar 54:55
Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza