Back to LanguagesPrevious ChapterNext Chapter EnglishArabicUrduHindiTamilBengali
Swahili - Chapter 87 - Al-Ala
Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink
Verse 1 — Surah Al-Ala 87:1
Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa
Verse 2 — Surah Al-Ala 87:2
Aliye umba, na akaweka sawa
Verse 3 — Surah Al-Ala 87:3
Na ambaye amekadiria na akaongoa
Verse 4 — Surah Al-Ala 87:4
Na aliye otesha malisho
Verse 5 — Surah Al-Ala 87:5
Kisha akayafanya makavu, meusi
Verse 6 — Surah Al-Ala 87:6
Tutakusomesha wala hutasahau
Verse 7 — Surah Al-Ala 87:7
Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana
Verse 8 — Surah Al-Ala 87:8
Na tutakusahilishia yawe mepesi
Verse 9 — Surah Al-Ala 87:9
Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa
Verse 10 — Surah Al-Ala 87:10
Atakumbuka mwenye kuogopa
Verse 11 — Surah Al-Ala 87:11
Na atajitenga mbali nayo mpotovu
Verse 12 — Surah Al-Ala 87:12
Ambaye atauingia Moto mkubwa
Verse 13 — Surah Al-Ala 87:13
Tena humo hatakufa wala hawi hai
Verse 14 — Surah Al-Ala 87:14
Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa
Verse 15 — Surah Al-Ala 87:15
Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali
Verse 16 — Surah Al-Ala 87:16
Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia
Verse 17 — Surah Al-Ala 87:17
Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi
Verse 18 — Surah Al-Ala 87:18
Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo
Verse 19 — Surah Al-Ala 87:19
Vitabu vya Ibrahimu na Musa