Back to Languages

Swahili - Chapter 88 - Al-Ghashiyah

Translation by Ali Muhsin Al Barwani — Permalink

Verse 1 — Surah Al-Ghashiyah 88:1

Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza

Verse 2 — Surah Al-Ghashiyah 88:2

Siku hiyo nyuso zitainama

Verse 3 — Surah Al-Ghashiyah 88:3

Zikifanya kazi, nazo taabani

Verse 4 — Surah Al-Ghashiyah 88:4

Ziingie katika Moto unao waka

Verse 5 — Surah Al-Ghashiyah 88:5

Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka

Verse 6 — Surah Al-Ghashiyah 88:6

Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba

Verse 7 — Surah Al-Ghashiyah 88:7

Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa

Verse 8 — Surah Al-Ghashiyah 88:8

Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu

Verse 9 — Surah Al-Ghashiyah 88:9

Zitakuwa radhi kwa juhudi yao

Verse 10 — Surah Al-Ghashiyah 88:10

Katika Bustani ya juu

Verse 11 — Surah Al-Ghashiyah 88:11

Hawatasikia humo upuuzi

Verse 12 — Surah Al-Ghashiyah 88:12

Humo imo chemchem inayo miminika

Verse 13 — Surah Al-Ghashiyah 88:13

Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa

Verse 14 — Surah Al-Ghashiyah 88:14

Na bilauri zilizo pangwa

Verse 15 — Surah Al-Ghashiyah 88:15

Na matakia safu safu

Verse 16 — Surah Al-Ghashiyah 88:16

Na mazulia yaliyo tandikwa

Verse 17 — Surah Al-Ghashiyah 88:17

Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa

Verse 18 — Surah Al-Ghashiyah 88:18

Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa

Verse 19 — Surah Al-Ghashiyah 88:19

Na milima jinsi ilivyo thibitishwa

Verse 20 — Surah Al-Ghashiyah 88:20

Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa

Verse 21 — Surah Al-Ghashiyah 88:21

Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji

Verse 22 — Surah Al-Ghashiyah 88:22

Wewe si mwenye kuwatawalia

Verse 23 — Surah Al-Ghashiyah 88:23

Lakini anaye rudi nyuma na kukataa

Verse 24 — Surah Al-Ghashiyah 88:24

Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa

Verse 25 — Surah Al-Ghashiyah 88:25

Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao

Verse 26 — Surah Al-Ghashiyah 88:26

Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao